Searching...
Monday, June 28, 2010

Cannavaro: Hatuna bahati na Afrika

Fabio Cannavaro
NAHODHA wa timu ya soka ya Italia, Fabio Cannavaro amesema kikosi cha timu hiyo maarufu kama Azzuri hakina bahati na bara la Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mechi yao dhidi ya Slovakia waliyolala kwa mabao 3-2 na kuvuliwa ubingwa, Cannavaro alisema, “inawezekana hatuna bahati hapa”.

Beki huyo wa kati wa Juventus alisema kuwa, hii ni mara ya pili wanashiriki michuano mikubwa barani Afrika wakiwa na kocha na kikosi bora lakini wanashindwa kufanya vizuri.

“Nashindwa kuwa najibu ambalo ninaweza nikalitoa liwaridhishwe nyie pamoja na mimi, naweza kusema mkaridhika lakini mimi nikawa sijaridhika. Sijui niseme nini hasa, nafikiri hatuna bahati hapa.

“Kikosi chetu ni bora, kila idara na utaona watu walicheza kwa nguvu na kutaka timu isonge mbele. Hakuna mchezaji hata mmoja angekubali kuona tunavuliwa ubingwa katika hatua hii, tena kwa kipigo kutoka kwa Slovakia.

“Tayari imetokea, si vibaya kusema tumewaangusha Wataliano waliofika hapa Afrika Kusini na waliobaki nyumbani lakini wakaendelea kutuunga mkono,” alisema Cannavaro baada ya kipigo hicho kwenye Uwanja wa Ellis Park katika jiji hili.

Mara ya kwanza, Italia ilishiriki michuano ya Kombe la Mabara jijini hapa, lakini ikaondolewa kwa kipigo cha aibu cha mabao 3-0 ilipokutana na Brazil ambao baadaye waliibuka na kuwa mabingwa.

Lakini kama hiyo haitoshi, katika michuano hiyo ya Mabara, Azzuri ilikutana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa mabingwa wa Afrika, Misri tena kwenye Uwanja huo huo wa Ellis Park.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!