Mji wa Barcelona wa nchini Uhispania unaonekana utajiunga na baadhi ya miji ya nchi za Ulaya iliyopiga marufuku vazi la niqab na burqa katika majengo ya serikali na tayari wanaharakati wa haki za binaadamu wamejipanga kukabiliana kisheria na jambo hilo.Tayari miji mingine mitatu ya Uhispania ya Catalonia, El Venrell na Lerida imeshachukua uamuzi kama huo wa kuwapiga marufuku wanawake wa Kiislamu kuvaa mavazi hayo.
Hata hivyo hatua hizo zinalalamikiwa vikali na mashirika ya haki za binaadamu barani Ulaya yakisisitiza kuwa, kufanya hivyo ni kukanyaga haki na uhuru wa watu kuvaa mavazi wanayopenda.
Licha ya kudai kustaarabika na kuwa na demokrasia, lakini nchi za Ulaya ziko tayari kuvumilia wanawake kutembea nusu uchi katika mitaa ya miji ya nchi hizo kuliko kuruhusu wanawake kujisitiri vizuri.
Miongoni mwa nchi za Ulaya zilizowahi kuchukua hatua kama hizo ni Ufaransa na Ubelgiji.


0 comments:
Post a Comment