Searching...
Tuesday, June 15, 2010

Maharamia wa Somalia wavunja rekodi ya idadi ya mateka katika mwaka huu

Shirika la utoaji msaada wa mabaharia SAP tarehe 14 huko Mombasa lilitoa takwimu mpya zikionesha kuwa, tokea mwaka huu uanze meli za nchi za nje zilizotekwa na maharamia wa Somalia zimezidi 20 na watu waliowateka nyara wamezidi 400, hali ambayo imeweka rekodi mpya ya idadi ya meli na mateka waliotekwa nyara na maharamia wa Somalia.

Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Andrew Mwangura alisema, walizitengeneza upya baadhi yameli walizoteka na kuzitumia katika kufanya mashambulizi dhidi ya meli nyingine za nchi za nje ili kuwababaisha mabaharia wa meli hizo. Bw. Mwangura aliitaka jumuiya ya kimataifa ifanye juhudi zaidi ili kutatua suala la maharamia wa Somalia.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!