Searching...
Monday, June 21, 2010

Jumba la UN la Expo2010 lafanya shughuli za siku ya wakimbizi duniani

Tarehe 20 Juni ni siku ya wakimbizi duniani. Jumba la Umoja wa Mataifa la Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai limefanya shughuli husika ili kuwakumbusha watu wafuatilie hali ya wakimbizi.

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limeeleza hali ya maisha ya wakimbizi wanaoishi mijini duniani na ugumu wa kazi zao kupitia maonesho ya picha na filamu, na kuwataka watu wafuatilie hali ya wakimbizi hao.

Mwezi Desemba mwaka 2000, baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuamua tarehe 20 Juni kuwa siku ya wakimbizi duniani kuanzia mwaka 2001, ili kuwakumbusha watu wafuatilie hali gumu ya maisha ya wakimbizi duniani.

Habari zaidi bofya hapa

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!