Ripoti mpya kuhusu mfumo wa biashara Afrika inaonya kuwa kukuwa kwa maingiliano ya biashara na nchi kubwa zilizoendelea zikiwemo China, India, na Brazil, hakujalisaidia bara hilo kusafirisha bidhaa zinazoliongezea faida.
Ripoti hiyo mpya ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na maendeleo UNCTAD inasema ongezeko la ushirikiano wa kibiashara eneo la Kusini kunaweza kulisaidia bara la Afrika sio tuu kwa kukuza biashara na kiwango cha fedha lakini pia kusaidia miundombinu ya eneo hilo na kuwapa ujuzi na teknolojia.


0 comments:
Post a Comment