Searching...
Monday, June 21, 2010

Drogba: Afrika tunajiondoa wenyewe mapema

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amesema iwapo timu za Afrika zitatolewa mapema kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea, basi hazina haja ya kutafuta mchawi.

Akizungumza na Championi Jumatatu uso kwa uso kwa mara nyingine tena jijini hapa, Drogba amesema karibu kila mechi timu ya Afrika iliyocheza imeonyesha uwezo wa karibu kila sehemu, lakini kumekuwa na mambo kadhaa yanayokuwa kama ugonjwa.

“Ninaweza kusema nikachukuliwa tofauti, unajua hata mimi bado niko mashindanoni, sijui nini kitatokea mbele kwa Ivory Coast ambayo ninaiongoza. Lakini hakuna haja ya kumtafuta wa kumlaumu mtu kama tukitolewa mapema, labda kitokee kitu kingine mbele.

“Timu za Afrika zimeonyesha uwezo mkubwa, ni vigumu kukuta timu ya Afrika imecheza mechi na kuzidiwa uwezo. Lakini mwisho itakuwa ni sare au imefungwa, tunajiangusha wenyewe. Tunatakiwa kuongeza umakini.

“Hakuna kitu cha mpira kinachotabirika, lakini pia kama kunakuwa na umakini uhakika unaongezeka zaidi. Afrika ina wachezaji bora kabisa na ndiyo chachu ya mafanikio ya timu nyingi za Ulaya, kuna kila sababu ya kusonga mbele zaidi,” alisema Drogba ambaye kwa mara ya kwanza alipotua nchini alizungumza na gazeti hili.

Drogba ambaye alipokuja nchini alifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na Championi pekee, alisema bado ana imani kubwa ya mabadiliko katika hatua za mwisho kwa timu za Afrika kusonga hadi hatua ya 16 bora na baadaye kuendelea mbele.

Katika michuano ya Kombe la Dunia, Afrika inawakilishwa na wenyeji Afrika Kusini, Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria na Cameroon hata hivyo zinaonekana kusuasua wakati hatua za awali za makundi zikienda ukingoni.
Habari na Globalpublisher

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!