Searching...
Thursday, June 24, 2010

China yaanzisha shule ya watoto yatima Zimbabwe

Bw. Xin Shunkang na Bibi Grace Mugabe

Kutokana na mwaliko wa mke wa rais wa Zimbabwe Bibi Grace Mugabe baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wa China nchini Zimbabwe tarehe 22 walitembelea nyumba ya watoto yatima ya mfuko wa fedha wa Grace Mugabe. Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Xin Shunkang alisema, serikali ya China itajenga shule moja itakayogharimu dola milioni 7 za kimarekani katika nyumba hiyo.

Bw. Xin Shunkang alisema, shule hiyo si kama tu itaweka mazingira mazuri kwa masomo ya watoto yatima, bali pia itawakaribisha watoto wanaokaa pembezoni mwa sehemu hiyo. Aidha Bw. Xin Shunkang anaeleza matumaini ya kuanzisha masomo ya lugha ya kichina katika shule ya msingi ili kujenga daraja la urafiki kati ya China na Zimbabwe.

Nyumba ya watoto yatima

bweni

jikoni

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!