Searching...
Friday, June 25, 2010

Bunge la Kenya lapitisha sheria inayoipa serikali uwezo wa kudhibiti bei

Sample ImageBunge la Kenya limeidhinisha sheria inayoipa serikali uwezo wa kudhibiti bei za bidhaa muhimu kama vile chakula na mafuta ya petroli. Sheria hiyo ambayo ilikuweko huko nyuma lakini ikaondolewa katika mwongo wa 90 itaipa serikali nguvu ya kuzuia wafanya biashara kupandisha ovyo bei za bidhaa muhimu kama wanavyofanya hivi sasa. Mwanabiashara atakayepatikana akiongeza bei za bidhaa bila ya idhini ya serikali atachukuliwa hatua kali za kisheria. Serikali imekaribisha hatua hiyo ikisema kuwa waliokuwa wakijitajirisha kwa njia isiyo ya halali sasa hawana tena nafasi hiyo. Hata hivyo mawaziri wengi wa serikali wamepinga sheria hiyo wakisema kuwa inatishia mustakabali wa uchumi wa nchi hiyo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!