Searching...
Sunday, May 23, 2010

Waziri Mkuu wa Kenya awasili Misri kujadili kadhia ya Mto Nile

Sample ImageWaziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amewasili Cairo kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa Misri kuhusu kadhia ya Mto Nile.
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga anatazamiwa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri Ahmad Nadhif kuhusu kadhia ya Mto Nile.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia anatazamiwa kuitembelea Misri na kufanya mazungumzo na Rais Husni Mubarak kuhusu suala la Mto Nile. Hivi karibuni baadhi ya nchi za kanda ya Mto Nile zilitia sainia mkataba kuhusu utumiaji wa Mto Nile. Mkataba huo utaziruhusu nchi hizo kuwa na matumizi ya maji zaidi ya kile kipimo kilichozikwaza nchi za Misri na Sudan chini ya mkataba wa mwaka 1959. Hatua hii inapingwa vikali na Misri pamoja na Sudan. Nchi zilizotia saini mkataba huo ni Tanzania, Rwanda, Ethiopia , Uganda na Kenya. Wakuu wa Cairo wanafanya mazungumzo na nchi husika ili kutatua mgogoro ulioibuka kuhusu Mto Nile.
Habari na Idhaa ya kiswahili redio tehran

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!