
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 22 huko Istanbul alisema suala la uharamia limekuwa ni tataizo kubwa kimataifa kwa usalama wa usafiri wa meli, ambalo limeifanya hali ya Somalia kukumbwa na msukosuko. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kupambana vikali na maharamia ili wakamatwe.
Bw. Ban Ki-moon alipohutubia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia alisema Umoja wa Mataifa utatangaza taarifa husika ya kuwakamata maharamia ili wahukumiwe. Alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa iiunge mkono Somalia katika mapambano dhidi ya maharamia, na kutaka usafiri wa meli utoe mchango mkubwa.
Rais Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia alisema vita nchini Somalia vimeleta hasara kubwa kwa jamii, shughuli za uharamia zinatokea mara kwa mara, na Somalia inahitaji msaada wa jumuiya ya kimataifa.


0 comments:
Post a Comment