Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamewachagiza mataifa kuidhinisha mikataba miwili kulinda haki za watoto_ Uuzaji wa watoto, ukahaba wa watoto na picha za ngono , na ulinzi wa watoto wakati wa vita.
Hayo ymechagizwa katika mkutano maalum uliofanyika leo katika ofisi za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF hapa New York.
Kampeni yenye lengo la kuyashawishi mataifa yote kuidhinisha mikatab hiyo ifikapo mwaka 2012 imetangazwa katika mkutano uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, Mkurugenzi wa UNICEF Anthony Lake, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika vita Radhika Coomaraswamy, na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa wa dhulma dhidhi ya watoto Marta Santos Pais.
Mikataba hiyo mawili inaupa uzito mkataba wa haki za Watoto , ambao leo unaadhimisha miaka kumi tangu upitishwe. Mkataba wa kuhusishwa watoto katika vita umeidhinishwa na mataifa 132, huku mataifa 25 yakisaini lakini bado kuuridhia na mataifa mengine 36 bado hayajaidhinisha wala kutia saini mkataba huo
0 comments:
Post a Comment