Searching...
Wednesday, May 26, 2010

Balozi wa China ahudhuria Mazungumzo ya Baraza la Afrika


Balozi wa China katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Bw. He Yafei tarehe 25 alishiriki kwenye Mazungumzo ya Baraza la Afrika (African Forum for Dialogue) yaliyofanyika huko Geneva.

Balozi huyo alizumgumzia uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Afrika na China akisema:

"China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, na Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, na ushirikiano kati ya China na Afrika ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa kusini na kusini. Hivyo kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuunga mkono amani na maendeleo ya Afrika ni sera ambayo China inafuata kithabiti."

Mazungumzo ya Baraza la Afrika yalianzishwa mwaka 2009 huko Geneva na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Jean Ping. Kauli mbiu ya mazungumzo ya mwaka huu ni "Amani na Maendeleo ya Afrika Yasukuma Mbele Maendeleo Endelevu". Watu wapatao 300 walishiriki kwenye mazungumzo hayo, wakiwa ni pamoja na wajumbe kutoka nchi za Afrika, Shirika la Mkutano wa Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa, na wajumbe wa China, Marekani, Japan, Russia na nchi nyingine katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!