Viongozi wa Afrika watakiwa kugawa rasilimali za nchi kwa uadilifu
Kamati ya watu mashuhuri wanaofuatilia maendeleo ya bara la Afrika imewataka viongozi wa Kiafrika kusambaza raslimali za nchi zao kwa uadilifu ili bara hilo liweze kufikia kilele cha saada na ufanisi. Kamati hiyo inayoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan imesema kwenye ripoti yake ya kila mwaka kuwa, ufisadi na uongozi mbaya ni miongoni mwa sababu zinazochangia bara la Afrika kubaki nyuma kimaendeleo. Akizungumza wakati wa kutolewa ripoti hiyo mjini Johannesburg Afrika Kusini, Kofi Annan amesema kuwa baadhi ya viongozi hawataki raslimali za nchi ziwafikie watu maskini na kutokana na hali hiyo umasikini umeendelea kulisakama bara hilo miaka nenda miaka rudi. Amewasihi viongozi waongozwe na uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao kwa raia.
0 comments:
Post a Comment