Searching...
Wednesday, May 26, 2010

Kasisi atiwa mbaroni Italia kwa tuhuma za kumlawiti kijana mdogo

Sample ImageKasisi mmoja mwenye umri wa miaka 73, ametiwa mbaroni mjini Milan Italia akikabiliwa na tuhuma za kumharibu kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu kijana mmoja raia wa kigeni akiwa na umri mdogo. Dormenico Pezzini wa Dayosisi ya Lodi alitiwa nguvuni juzi akituhumiwa kuwa alikuwa akimharibu kijana huyo kuanzia alipokuwa na umri wa miaka 13 hadi 16. Inasemekana kuwa muathirika huyo ambaye hivi sasa ameshakuwa mtu mzima alikuwa akisaidiwa kifedha na kasisi huyo. Wakati alipofanyiwa upekuzi nyumbani kwake, Pezzini alikutwa na vitu vya ponografia. Kasisi huyo ni maarufu katika duru za watu wanaolawitiana, akiwa anajulikana kama mratibu wa makundi ya watu hao wanaofanya utafiti juu ya suala la dini na maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja. Katika siku za hivi karibuni, Vatican imekuwa ikishambuliwa vikali kwamba Kanisa lake Katoliki limekuwa kwa miaka mingi likiwalinda makasisi wanaohusika na vitendo vya liwati, ambapo badala ya kuhakikisha wanafunguliwa mashtaka limekuwa likichukua hatua za kuwahamisha tu kutoka Parokia moja hadi nyingine.../

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!