Searching...
Thursday, May 27, 2010

Rais Hu Jintao wa China afanya mazungumzo na rais Patil wa India

Rais Hu Jintao wa China tarehe 27 hapa Beijing amekuwa na mazungumzo na rais Pratibha Patil wa India ambaye yuko ziarani nchini China.

Rais Hu amesema, rais Patil siku zote anatilia maanani uhusiano kati ya India na China, kutetea kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizi mbili, na kuhimiza uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na India uendelezwe zaidi. Rais Hu ameeleza imani yake kuwa ziara ya rais huyo hakika itaongeza maelewano na urafiki kati ya China na India na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa nchi hizi mbili.

Rais Patil wa India amesisitiza tena kuwa, India inapenda kuhimiza zaidi uhusiano wa nchi mbili ulio wa masikilizano, urafiki na wenye nguvu ya uhai uendelezwe siku hadi siku.

Habari nyingine zinasema kuwa, spika wa bunge la umma Bw. Wu Bangguo na waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao siku hiyo pia wamekutana na rais wa India Bibi Pratibha Patil.

Idhaa ya Kiswahili Redio China

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!