Ofisa wa shirikisho hilo Bw. David Machay siku hiyo amesema, uchumi wa nchi mbalimbali za Afrika Mashariki zikiwemo Kenya, Tanzania na Uganda umeathirika vibaya kutokana na shughuli za uharamia. Aidha malipo ya bima ya meli yanaongezeka, na gharama za usafirishaji kwa njia ya meli pia zimepanda kutokana na makampuni ya meli kukodi meli za kufanya ulinzi.
Bw. Mackay alisema endapo jumuiya ya kimataifa haitachukua hatua za kuzuia na kupambana na uharamia nchini Somalia, mchakato wa kuendeleza viwanda katika nchi za Afrika Mashariki utaathiriwa vibaya.
0 comments:
Post a Comment