Searching...
Thursday, May 27, 2010

Nchi za Ulaya zajipanga kukabiliana na umaskini barani humo


Sample ImageUmoja wa Ulaya umetangaza kuwa, wakazi milioni 80 wa nchi wanachama wa umoja huo wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Taarifa ya umoja huo imesema, kati ya kila watu 7 nchini Ujerumani, mmoja anaishi chini ya mstari wa umaskini.
Ni kwa sababu hiyo ndio maana umoja huo umeutangaza mwaka huu wa 2010 kuwa ni Mwaka wa Kupambana na Umaskini na Kutengwa katika Jamii.
Takwimu zinaonesha kuwa, karibu asilimia 14 ya Wajerumani wanaishi chini ya mstari wa umaskini.
Miongoni mwa ratiba za umoja huo za kukabiliana na mgogoro huo ni kujaribu kuongeza kiwango cha elimu cha wakazi wa nchi wanachama.
Ijapokuwa wataalamu barani Ulaya wamelipokea vizuri suala la kusaidiwa kifedha Wazungu maskini, lakini hawaamini kuwa kupandishwa kiwango cha mishahara na kutolewa misaada ya kifedha na serikali kwa ajili ya watoto, kutasaidia kutatua tatizo hilo sugu na ndio maana Umoja wa Ulaya unajaribu kutumia mbinu ya kuelimisha na kutoa mafunzo kama silaha kuu ya kupambana na umaskini huko Ulaya.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!