Wafanyakazi Afrika Kusini watishia kugoma wakati wa kombe la dunia
Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini COSATU umetishia kuitisha mgomo wa nchi nzima wakati wa mashindani ya kombe la dunia katika mchezo wa soka yanayotarajiwa kuanza Juni 10. Katibu Mkuu wa COSATU Nzwelinzima Vavi amesema kuwa mgomo huo huenda ukafanyika kutokana na kupanda bei ya umeme kiasi kwamba wananchi wa kawaida hawawezi kumudu gharama yake. Vavi amesema kuwa mkutano kati ya muungano huo na baraza la kushughulikia uchumi na maendeleo utafanyika Juni 14 na iwapo hakutopatikana natija yoyote kwenye mkutano huo basi mgomo huo utafanyika. Afrika Kusini itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuaanda dimba la kombe la dunia katika mchezo wa soka.
0 comments:
Post a Comment