Searching...
Monday, May 24, 2010

Nairobi-Kenya kutenga dola za kimarekani milioni 26 kutangaza shughuli zake za utalii duniani

Shirikisho la utalii la Kenya tarehe 23 lilitoa taarifa likisema kuwa mwaka huu shirikisho hilo litatenga shilingi za Kenya bilioni 2 kwa ajili ya kutangaza shughuli zake za utalii duniani, ili kuwavutia watalii wengi watembelee Kenya.

Shirikisho la utalii lilisema Kenya ni sehemu maarufu ya utalii duniani, ina vivutio vya kipekee vya mazingira ya asili, hoteli nyingi za kifahari na zana na vifaa vya hali ya juu. Vurugu zilizotokea mwishoni mwa mwaka 2007 vilisababisha hasara kubwa kwa sekta ya utalii ya Kenya. Shirikisho hilo litaongeza nguvu ya kutangaza shughuli zake za utalii ili kuwavutia watalii wengi.

Mwaka 2009, mapato ya shughuli za utalii za Kenya yalikuwa ni dola za kimarekani milioni 830. Shirikisho la utalii la Kenya lilikadiria kuwa kutokana na kufufuka kwa uchumi wa dunia, hali ya siasa nchini Kenya kuelekea kuwa ya utulivu na msukumo wa kutangaza shughuli za utalii za Kenya duniani, pato la shughuli za utalii za Kenya litaongezeka kwa asilimia 8 mwaka 2010.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!