Mazungumzo ya duru ya pili kati ya China na Marekani kuhusu mikakati na uchumi yamefunguliwa tarehe 24 hapa Beijing. Rais Hu Jintao wa China amehudhuria ufunguzi wa mazungumzo na kutoa hotuba. Rais Obama wa Marekani ameleta risala ya maandishi.
Rais Hu Jintao alipotoa hotuba alisema, China na Marekani zinapaswa kushikilia mwelekeo sahihi wa uhusiano wa China na Mareakani, kuheshimu maslahi muhimu na ufuatiliaji mkubwa wa kila upande, kuheshimu haki ya kila nchi ya kujiamulia njia yake ya kujiendeleza, kudumisha mawasiliano kati ya viongozi na watu wa ngazi mbalimbali, kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha uratibu katika masuala ya kikanda na kimataifa, na kuongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa China na Marekani.
Risala ya maandishi ya rais Obama inasema, Marekani na China zikiwa makundi mawili makubwa zaidi ya uchumi duniani, zinapaswa kushirikiana na wanachama wa kundi la nchi 20 katika kuhimiza ufufukaji wa uchumi wa dunia nzima, na kukabiliana kwa pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na kutatua masuala ya kikanda na kimataifa. Mazungumzo kati ya Marekani na China kuhusu mikakati na uchumi yanasaidia pande hizi mbili kuongeza mawasililano na maelewano. Marekani inapenda kufanya juhudi pamoja na China katika kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kwenye mambo mbalimbali.


0 comments:
Post a Comment