Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa dunia kuchukua mtazamo mpya ili kusaidia kuleta amani nchini Somalia.
Ban ametoa wito huo kwenye mkutano wa kimataifa wa kuhusu Somalia nchi iliyoko kwenye pembe ya Afrika , na amesema kwa kushindwa kuchukua hatua sasa kuna hatari ya machafuko ya Somalia kuingia kwa jirani zake na kwengineko. Ban amesema kitu kimoja ambacho ni dhahiri ni kwamba, kama hatutabadili mtazamo basi kutakuwa na fursa ndogo sana ya kuleta amani Somalia.
Amesema watu milioni 3.2 wanahitaji msaada wa kibinadamu haraka , na pia kutoa taswira ya kisheria ya kuwafikisha mahakamani maharamia wanaosumbua pwani ya Somalia. Mbali ya hayo amesisitiza ujenzi mpya wan chi hiyo iliyosambaratishwa na vita kwa kuwashirikisha jamii ya wafanya biashara wa Kisomali walioko nyumbani na nje ya nchi.
Mkutano huo wa siku tatu uliofanyika Istanbul na kufadhiliwa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Uturuki umekuwa ukitathimini siasa za Somalia, usalama, na mahitaji ya ujenzi mpya mwaka mmoja baada ya mkutano kama huo kufanyika Brussels.
0 comments:
Post a Comment