Searching...
Tuesday, May 25, 2010

Cairo-Mgao wa maji ya mto Nile wa Misri hautabadilika

Waziri mkuu wa Misri Bw. Ahmad Nazif tarehe 24 alisema makubaliano ya maliasili ya maji ya mto Nile hayatabadili mgao wa maji ya mto huo wa Misri.

Siku hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa pamoja na Bw. Nazif na waziri mkuu wa Kenya Bw. Raila Odinga ambaye yuko ziarani nchini Misri, Bw. Nazif alisema viongozi wote wa nchi zilizopo kwenye eneo la mtiririko wa mto Nile walisema kuwa hawana uhasama na Misri, hali ambayo inaonesha kuwa mgao wa maji ya mto Nile wa Misri hautabadilika.

Bw. Nazif alisema miradi yoyote inayohusika na mto Nile inapaswa kuwasilishwa kwa nchi zilizopo kwenye eneo la mtiririko wa mto huo ili ijadiliwe.

Bw. Odinga alisema sehemu zinazoleta utata kwenye makubaliano mapya zitaendelea kujadiliwa hadi pande mbalimbali zitakapokubali kabisa.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!