Searching...
Tuesday, May 25, 2010

New York-Umoja wa Mataifa hautaacha kuisaidia Somalia kutatua tatizo lake

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 24 alisema Umoja wa Mataifa hautaacha kuisaidia Somalia kutatua tatizo lake, na taarifa ya Istanbul iliyofikiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Somalia imeonesha nia hiyo ya umoja huo.

Bw. Ban Ki-moon aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkutano huo ni muhimu kwa Somalia ambayo iko kwenye kipindi muhimu, na kwenye mkutano huo, jumuiya ya kimataifa imesema itaunga mkono serikali ya Somalia kwa pande zote.

Bw. Ban Ki-moon alisema taarifa hiyo imeonesha wazi kuwa Umoja wa Mataifa hautaacha kuisaidia Somalia kutatua tatizo lake, lakini serikali ya mpito ya Somalia inapaswa kutekeleza wajibu wake wa kushughulikia suala la usalama, na kama matatizo nchini Somalia ambayo ni chanzo cha uharamia hayatatatuliwa, suala la maharamia halitatokomezwa kamwe.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!