Kulingana na matokeo yaliyotolewa Jumanne, asilimia 54 ya Wakenya wanapendelea ICC iendeshe kesi hizo badala ya mahakama za ndani ya Kenya.
Miongoni mwa wale wanaopinga uingiliaji wa ICC nusu wanasema wanataka watuhumiwa wafanyiwe kesi na mahakama za ndani ya nchi, na nusu wanasema ni bora wasamehewe.
Jumapili, Waziri wa Sheria wa Kenya, Mutula Kilonzo, alizusha mzozo alipopendekeza kuwa Kenya inaweza kuendesha kesi dhidi ya watuhumiwa hao kwa kupitia taasisi zilizoundwa na katiba mpya ya Kenya.
Matamshi ya Kilonzo yalipingwa vikali na makundi ya haki za binadamu na hata maafisa wengine wa serikali.
0 comments:
Post a Comment