"Hakuna sababu Afrika isiwe muuzaji mkubwa wa chakula nje," Obama
Akihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York Alhamisi rais Obama alisema "hakuna sababu Afrika isiwe muuzaji mkubwa wa chakula nje." Aliongezea kuwa ndio sababu ameweka mipango nchini mwake ambaye itawezesha wakulima barani Afrika.
Alisema Marekani inafanya juhudi kuifanya dunia iwe wazi zaidi, na kuwezesha biashara na kuinua uchumi wa nchi zote duniani kwa ushirikiano katika nyanja zote. Alisema hakuna sababu kwa mfanyabiashara kulipa rushwa akitaka kufungua biashara, na kukumbusha kuwa wajibu wa serikali ni kuwezesha wananchi sio kuwabana.
0 comments:
Post a Comment