Searching...
Thursday, September 23, 2010

China kusamehe madeni ya nchi zilizoko nyuma zaidi duniani

China itasamehe madeni ya nchi zilizoko nyuma zaidi kiuchumi duniani, ili kuzisaidia hizo kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.
Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao tarehe 22 alipohudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia, alielezea kuwa, katika miaka mitatu ijayo, China itatoa michango ya fedha ya dola za kimarekani milioni 14 kwa mifuko ya Ukimwi, TB na Malaria duniani, itasamehe madni ya nchi 50 ambazo zina madeni mengi na zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo duniani, pia itatoa msaada mwingine wa dola za kimarekani milioni 200 kwa sehemu zilizokumbwa na mafuriko nchini Pakistan.
Aidha Bw. Wen Jiabao ameitaka jumuiya ya kimataifa kutoa kipaumbele katika suala la maendeleo na upunguzaji wa umaskini kwa nchi za Afrika, ili kuhakikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanatimizwa kabla ya mwaka 2015.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!