Jamii ya kimataifa imeendelea kulaani mpango wa kasisi Terry Jones wa kanisa la Kiangikana la Marekani wa kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani kushokutwa tarehe 11 Septemba.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu mpango wa kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani akisisitiza kuwa hatua hiyo haiwezi kukubaliwa katika dini yoyote ile. Vilevile Umoja wa Ulaya umepinga vikali mpango huo wa kasisi wa kanisa la Kiangikana katika jimbo la Florida.
Jana Kiongozi wa Wakatoliki Duniani Papa Benedict wa 16 alikemea vikali mpango huo akisema kuwa ni dharau kubwa. Taarifa ya Vatican imesema kuwa kuchoma moto kitabu kitakatifu ni kitendo hatari mno kitakachochea chuki.
Kasisi Terry Jones wa kanisa Dove World Outreach Center huko Marekani ameushambulia Uislamu akiutaja kuwa ni kazi ya shetani na amewataka wafuasi wake kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani tarehe 11 Septemba mwaka huu katika kumbukumbu ya mashambulizi ya New York na Washington mwaka 2001.
0 comments:
Post a Comment