Searching...
Thursday, September 9, 2010

Obama atangaza mpango mwingine wa kuinua uchumi

Rais Barack Obama  (AP Photo/J. Scott Applewhite)
Rais Barack Obama
Vyombo vya habari Marekani vinawakariri  maafisa  wakisema kuwa rais Barack Obama anapanga kupendekeza nafuu ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wiki hii.
Bwana Obama anatazamiwa kutangaza mpango huo Jumatano huko Cleveland, Ohio, ambao utaruhusu biashara kutoa asilimia 100 ya gharama ya uwekezaji mpya kutoka kwenye kodi zao mpaka 2011.
Mpango huo unategemewa kugharimu zaidi ya dola bilioni 200 katika miaka miwili ijayo . Bwana Obama pia anatazamiwa  kutangaza mapendekezo yatakayowezesha kupunguza kodi moja kwa moja kwa utafiti wa biashara na maendeleo.
Mapendekezo hayo yatakuwa ni juhudi ya hivi karibuni ya Obama kupambana na ongezeko la ukosefu wa kazi Marekani, wiki chache kabla ya upigaji kura wa bunge mwezi November.
Jumatatu rais alipendekeza mpango wa miaka 6 wa dola bilioni 50 ili kujenga upya barabara za nchi, reli na viwanja vya ndege wakati wa hotuba yake kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanachama wao mjini Milwaukee, Wisconsin.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!