Searching...
Friday, September 24, 2010

Wanawake wanaovaa hijabu ya Kiislamu wakandamizwa Ujerumani

 Sample ImageBi. Hamida Muhaqiqi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Paderborn nchini Ujerumani amekosoa vikali vitendo vya kibaguzi vinavyofanywa dhidi ya wanawake wa Kiislamu nchini Ujerumani. Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya wanasheria nchini Ujerumani, Bi Muhaqiqi ameongeza kuwa, wanawake wa Kiislamu nchini humo hawapati haki sawa ya kiajira. Mhadhiri huyo wa Chuo Kikuu cha Paderborn ameelezea ubaguzi huo dhidi ya wanawake wanaovaa hijabu kuwa umeshika mizizi na hasa kwenye shule za nchi hiyo. Ameongeza kuwa, uvaaji wa hijabu kwa wanawake wa Kiislamu ni jukumu la kidini mbele ya Mwenyezi Mungu. Hamida Muhaqiqi amesisitiza kuwa, hali ya wanawake wanaovaa hijabu nchini Ujerumani ni mbaya sana, kwani licha ya ubaguzi, wamekuwa wakidunishwa, kudhalilishwa na hata kutukanwa katika sehemu zao za kazi. Kwa mujibu wa sheria za Ujerumani, uvaaji wa hijabu ni marufuku kwenye idara za serikali nchini humo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!