Maafisa wanasema polisi walifyetua risasi baada ya wahamiaji kupuzi onyo la kusimama. Tukio hilo limeongeza idadi ya wahamiaji walouliwa kwenye mpaka huo kufikia 28 mwaka huu.
Makundi ya kutetea haki za binadam yamekosoa vikali Misri kwa kutiumia nguvu za kupindukia kuwazuia wahamiaji wasio na silaha wanaojaribu kuingia Israel.
Hapo mwezi Marchi Kamishna mkuu wa Haki za Binadam wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay alitoa wito wa kukomeshwa kile alichoikieleza ni “kitendo cha kulaaniwa” cha utumiaji nguvu wa kusababisha vifo, ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 60 tangu kati kati ya 2007.Bi. Pillay anasema idadi kubwa ya wahamiaji walouliwa walitokea nchi za Afrika, kusini mwa janga la Sahara, hasa Sudan, Ethopia na Eritrea.
0 comments:
Post a Comment