Searching...
Monday, September 13, 2010

BAADA YA CHAI KULIKUWA NA MTOKO NJE KIDOGO YA MJI WA HYDERABAD

Tulipowasili maeneo ya kujidai kama panavyoonekana panaitwa Pragat Resort ni nje kidogo ya mji huu wa Hyderabad
  Tulipata picha ya pamoja kama kumbukumbu kabla ya kuingia ndani
Mjomba Nass akiongoza kundi kuelekea ndani ni huyo alievaa begi kulia kwake ni Bw.Ally na kushoto kwake ni M/kiti wa jumuiya yetu ya hapa Hyderabad
Kijana Ally kama anavyoonekana akipata kumbukumbu mojawapo ndani ya Pragat Resort
Mjomba Nass nae akuwa nyuma katika swala zima la kupata kumbukumbu huku akifanya mawasiliano
 Tulichangamsha miili kwa kucheza michezo tofauti hapa nikiwa na wadau uwanjani tukicheza mpira wa miguu ilikuwa furaha sana siku hiyo
 Moja ya pirikapirika uwanjani
Kulikuwa na patashika nguo kuchanika siku hiyo vijana wanauwezo mkubwa sana uwanjani mwisho wa mchezo timu yangu ndio iliyoibuka na ushindi siku hiyo
 Mie kama ninavyoonekana baada ya kumaliza kazi uwanjani nikafanyiwa mabadiliko na wengine nao wapate kucheza hapa tayari tulikuwa tushashinda 4-1
 Ulifika wakati swimming kama anavyoonekana Bw.Ayoub
 Kiukweli wadau walishereheka sana ndani ya swimm huku stori zinaendelea zikiongozwa na Bw.Matata
 Hii ndio swimming iliyopo pragati resort kama inavyoonekana kwa juu mpiga picha wetu alivyoikamata taswira yote
 M/kiti akishangweka ndani ya maji na kupata taswira yake
 Kiukweli hii sehemu inavutia mno pametulia sana wadau wamepapenda sana uenda wakarudi tena eid ijayo
Bw.Abdul-aziz na Bw.Amir wakipata taswira ya pamoja ndani ya swimming wakiwa na rafiki yao
Mambo hayo palikuwa hapatoshi M/kiti akila miondoko ya kihindi katikati alienyoosha mikono
 Palikuwa na patashika pale mzuka ulipompanda unaweza kusema muhindi kweli anavyopatia mihondo ya kihindi
 Mashefa ya Tolichoki hayo kama yanavyooneka toka kushoto ni Bw.Alex a.k.a Chola akiwa sambamba na Bw.Blest a.k.a Big Boss wakipunga upepo ni baada ya kumalizika kwa shangwe.
 Kwa kweli sina budi kuishukuru timu nzima iliyoandaa mtoko huu wadau walifurahi sana mpaka kupelekea wadau kuiomba tena wakati ujao hili waweze  kurudi tena hapa, Urary95 blog inaishukuru sana timu nzima iliyokuwa chini ya Bw.Mustafa a.k.a Matata kwa kuweza kufanikisha mtoko huu bila ya kusahau timu nzima ya Blog hii ikiwa chini yangu.Ahsanteni
 






0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!