Searching...
Monday, September 20, 2010

Maelfu waandamana London kupinga safari ya Papa Benedict nchini Uingereza

Sample ImageMaelfu ya watu waliandamana jana mjini London kupinga safari ya Papa Benedict XVI nchini Uingereza wakimtaka Kiongozi wa Kanisa Katoliki kufichua majina ya makasisi waliohusika katika kashfa ya kuwanajisi watoto wadogo, kuweka wazi mafaili yao na kuwafikisha mahakamani.
Watu wasiopungua elfu 12 waliandamana jana katika mitaa ya London wakibeba mapango yanayolaani uhalifu wa makakasisi wa Kikatoliki na kutoa wito wa kulindwa watoto na si kuwakingia kifua makasisi.
Safari ya Papa Benedict XVI nchini Uingereza imeandamana na mashambulizi makali ya vyombo vya habari dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki na fedheha ya makasisi ya kuwanajisi watoto wadogo.
Maelfu ya askari usalama wa Uingereza wanashiriki katika operesheni ya kulinda amani ya Papa Benedict XVI ambayo imegharimu pauni milioni moja na nusu. Inakadiriwa kuwa gharama za safari ya Papa nchini Uingereza zitafikia pauni milioni 20 zikiwemo pauni milioni 12 za walipa kodi.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!