Searching...
Monday, September 20, 2010

Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi ya nchi 22 yapungua

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi, UNAIDS zinasema, kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2009 idadi ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ukimwi katika sehemu nyingi duniani inaendelea kupungua au iko katika hali ya kutulia, na idadi hiyo kwa nchi 22 za Afrika, kusini mwa Sahara zilizokuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi imepungua kwa asilimia 25.
Lakini takwimu hiyo pia zimeonesha kuwa hali ya maambukizi ya Ukimwi katika sehemu za mashariki mwa Ulaya na Asia ya kati inaendelea kuongezeka, katika nchi kadhaa tajiri maambukizi ya Ukimwi kati ya mashoga yanaongezeka.
Takwimu zinaonesha kuwa hivi sasa watu milioni 5.2 wanapata matibabu ya ugonjwa wa Ukimwi duniani, na mwaka 2008 idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa Ukimwi ilipungua kwa laki 2 ikilinganishwa na mwaka 2004.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!