Watu nusu milioni watembelea maonyesho ya Qurani Tehran
Zaidi ya watu nusu milioni hadi sasa wametembelea Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qurani Tukufu yanayoendelea katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini mjini Tehran. Maonyesho ya mwaka jana yalihudhuriwa na watu milioni moja na nusu na inatazamiwa kuwa washiriki katika maonyesho ya mwaka huu yatakayomalizika tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wataongozeka kwa asilimia 25. Mbali na mashirika 340 ya uchapishaji nchini Iran yanayoshiriki, vile vile kuna mashirika 15 ya kimataifa ya uchapishaji yanayoshiriki. Aidha kuna mashirika 90 ya programu za kompyuta kuhusu Qurani Tukufu yanayoshiriki katika maonyesho haya. Kuna nchi 28 zinazoshiriki katika maonyesho hayo katika kitengo cha Qurani na Mataifa ya Kiislamu. Maonyesho ya Kimataifa ya Qurani yanafanyika nchini Iran kwa lengo la kuhimiza utamaduni wa Qurani katika jamii.
0 comments:
Post a Comment