Serikali ya Afrika Kusini imepata idhini ya mahakama ya kuzuia mgomo wa wafanyakazi wanaotoa huduma muhimu.
Zaidi ya wafanyakazi milioni moja wa sekta ya umma wanaodai nyongeza ya mishahara walianza mgomo usio wa muda maalumu Jumatano iliyopita. Serikali imesema sekta zinazotoa huduma muhimu ni pamoja na mahospitali na magereza. Ijumaa Waziri wa Afya wa Afrika Kusini alisema wafanyakazi wa sekta nyeti ya afya wanaogoma watakabiliwa na mashtaka ya mauaji.
Vyama vya wafanyakazi vinataka nyongeza ya asilimia 8.6 ya mishahara pamoja na kodi ya nyumba ya dola 137. Hata hivyo serikali inasema ina uwezo wa kuongeza asilimia 7 na dola 96 tu za kodi ya nyumba.
0 comments:
Post a Comment