Waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani ametoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa dharura wa maafisa wa afya, viongozi wa majimbo na mashirika ya misaada ili kuratibu juhudi za kupambana na tishio linalozidi kuongezeka la kusambaa kwa magonjwa katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko nchini.
Hatua hiyo inafuatia kukosolewa kwa serikali na wananchi kuhusu jinsi ilivyoshughulikia janga hilo hadi sasa.Umoja wa Mataifa umeonya kuwa zaidi ya watoto millioni tatu walioathiriwa na mafuriko wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa na maradhi hatari yanayotokana na maji.
Taarifa zinasema kuwa juhudi za kimataifa za kupeleka misaada zilifanikiwa kupata millioni mia nne na tisini zilizoahidiwa kwa Pakistan, huku kukiwa na ahadi nyingine ya dola millioni mita tatu na ishirini na tano.
0 comments:
Post a Comment