Searching...
Sunday, August 22, 2010

Nairobi-Kenya yawahukumu Waethiopia 89 kwa kuingia kiharamu nchini humo

Idara ya uhamiaji ya Kenya tarehe 20 ilitoa taarifa ikisema, polisi wa Kenya wamewakamata Waethiopia 89 waliovuka mpaka na kuingia kiharamu nchini Kenya, na mahakama ya Kenya imewahukumu watu hao.
Ofisa mwandamizi wa sehemu ya Kibera mjini Nairobi amesema, Waethiopia hao wakiwemo wanawake wengi wenye umri wa kati ya miaka 18 na 45, walipatikana kwenye kitongoji cha Nairobi bila ya kuwa na kitambulisho au kibali chochote cha kuingia nchini Kenya.
Ofisa huyo amesema Waethiopia hao walikuwa wanataka kwenda Afrika Kusini na Malawi kwa kupitia nchini Kenya.
Polisi wa Kenya wamesema Waethiopia hao wamekiri hatia zao, na idara husika ya Kenya itawarejesha nyumbani katika siku chache zijazo.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!