Katibu mkuu Ban anasema ubakaji wa wanavijiji wa Congo, ulifanywa na wapiganaji wenye silaha wa makundi mawili ya waasi. Alieleza mashambulizi hayo kuwa mfano mwengine mbaya wa kiwango cha ghasia za ngono na ukosefu wa usalama unokumba Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky akisoma taarifa ya Bw. Ban amesema,
“Katibu mkuu anarudia wito wake wakutaka makundi yote yeney silaha huko DRC, kuweka chini silaha zao, na kuungana na utaratibu wa amani. Katibu mkuu pia anatoa wito kwa serikali ya congo kuchunguza tukio hilo na kuwafikisha wahusika wa uhalifu huo mbele ya sheria, na kuanzisha tena juhudi za kumaliza ukosefu wa usalama huko mashariki mwa nchi hiyo.”
Wakati huo huo Bw Ban anamtuma naibu Katibu Mkuu wa masuala ya kulinda amani Atul Khare, kwenda huko DRC kuchunguza mashambulizi hayo. Nae mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya ghasia za ngono Margot Wallstrom, amepewa jukumu la kusimamia namna Umoja wa Mataifa utakabiliana na tatizo hilo.
Anasema mashambulizi ya Kivu Kaskazini yanathibitisha uchunguzi wake wakati wa ziara yake ya hivi karibuni huko DRC, juu ya kuenea kwa mpangilio ubakaji na kiukaji mwengine wa haki za binadam nchini humo.
Kulingana na ripoti za habari, mashambulizi ya waasi yalifanyika baina ya tarehe 30 Juli na Agasti 3. Umoja Mataifa unasema kuwa una kambi dogo la kikosi cha amani takriban kilomita 30 kutoka kijiji hicho. Lakini kulingana na msemaji Martin Nersirky, waasi waliwafungia njia wanavijiji, na hawakuweza kwenda kuripoti mashambulizi kwa watu wa nje.
Kulingana na bw. Nersirky, walinda amani walipata habari za ubakaji huo kutoka kwa mfanyakazi wa huduma za afya hapo Ogasti 12, hiyo ikiwa ni wiki mbili baada ya tukio hilo kutendeka. Na kwamba ni juu ya serikaliya DRC kufanya uchunguzi wa
0 comments:
Post a Comment