Mtangazaji mmoja mkonsevativu katika televisheni za Marekani amezusha mzozo mkubwa kwa mipango yake ya kufanya mkutano wa hadhara siku ambayo kwa kawaida inaadhimisha hotuba maarufu ya mtetezi wa haki za binadamu Martin Luther King Jr. inayojulikana kama "I Have a Dream." Anapanga kufanya mkutano huo mahali ambapo King alitoa hotuba hiyo miaka 47 iliyopita.
Maelfu ya watu wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo ulioitishwa na mtangazaji huyo Glenn Beck Jumamosi mjini Washington mbele ya jumba la makumbusho la rais wa zamani wa Marekani Abraham Lincoln.
Waandaaji wa mkutano huo wanasema mkutano huo una lengo la kutoa shukurani kwa wanajeshi wa Marekani na watu wengine ambao "ni kioo cha misingi ya waanzilishi wa taifa ya hadhi, ukweli na heshima." Gavana wa zamani wa Alaska Sarah Palin anatazamiwa pia kuhudhuria mkutano huo.
Kwa upande mwingine, wanaharakati wa haki za raia pia wanapanga mkutano wa hadhara Jumamosi kuadhimisha hotuba hiyo muhimu ya Martin Luther King Jr. katika historia ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment