Katika habari iliyotolewa Alhamisi polisi wa kimataifa-Interpol wamesema oparesheni hiyo iitwayo Mamba III inawakilisha uchunguzi wa miezi miwili inayowalenga watu wanaoshukiwa kutengeneza, kusambaza na kuuza madawa bandia katika nchi za Burundi, Tanzania, Uganda, Kenya na Rwanda.
Interpol imesema uvamizi huo wa polisi ulifanyika kwa siku mbili katika Afrika ya Mashariki. Shirika hili limesema uchunguzi wao kwa ushirikiano na shirika la afya duniani na kikosi cha kupambana na vitu bandia unaendelea na oparesheni hiyo kupambana na madawa bandia ya kuzuia malaria, chanjo na Antibiotic. Interpoli pia ilisema maafisa walikamata kiasi kikubwa cha madawa ya serikali ambayo yaliingizwa kwa njia za panya.
0 comments:
Post a Comment