Milioni moja wengine hawana pa kuishi kutokana na mafuriko nchini Pakistan
Umoja wa Mataifa leo umesema kuwa watu wengine milioni moja hawana pa kuishi nchini Pakistan kutokana na mafuriko, huku maafisa wa Islamabad wakitoa amri mpya ya watu kuondolewa katika jimbo la kusini la Sindh. Stacey Winston Afisa wa Ofisi ya Upashaji habari na Kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Pakistan (UNOCHA) amesema kwamba zaidi ya watu milioni moja wengine wamepoteza makaazi yao katika masaa 48 yaliyopita kwenye eneno la Sindh. Taarifa hizo zimetolewa baada ya maji ya mto Indus kupasua kuta na kuelekea katika mji wa Thatta suala lililopelekea kutolewa amri ya watu kuuhama mji huo. Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za msimu zilizoanza mwishoni mwa mwezi uliopita wa Julai yamemeza maelfu ya vijiji na miji nchini Pakistan, kuharibu mamilioni ya hekta za kilimo na kuua zaidi ya watu
0 comments:
Post a Comment