Rais Mwai Kibaki wa Kenya asaini katiba mpya kuwa sheria
Rais Mwai Kibaki wa Kenya leo amesaini katiba mpya ya nchi hiyo iliyongojewa kwa muda mrefu na kuwa rasmi sheria, wiki kadhaa baada ya kupasishwa katika kura ya maoni. Tukio hilo limeshuhudiwa na umati mkubwa wa Wakenya waliohudhuria sherehe za kusainiwa katiba mpya zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Park jijini Nairobi. Katiba hiyo inayochukua nafasi ya katiba iliyopita iliyotayarishwa baada ya uhuru, ni utekelezwaji wa sehemu ya makubaliano ya viongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Kenya yenye lengo la kuzuia kutokea tena machafuko kama yale yaliyojiri baada ya uchaguzi wa Rais mwezi Disemba mwaka 2007. Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwepo Rais Omar al Bashir wa Sudan.
0 comments:
Post a Comment