Searching...
Monday, August 2, 2010

Jeshi la Marekani lakiri kuwa na mpango wa kuishambulia Iran


Mwenyekiti wa Baraza la wanadhimu wakuu wa jeshi la Marekani Jenerali Michael Mullen tarehe 1 Agosti aliposhiriki kwenye mahojiano ya kampuni ya NBC ya Marekani, alisema Marekani ina mpango wa kuishambulia Iran, lakini operesheni ya kijeshi siyo chaguo zuri zaidi kwa Marekani. Kwa sababu ya matokeo yake na matatizo mbalimbali yanayoweza kusababishwa na opresheni ya kijeshi.

Kwa maoni yake, juhudi za kidiplomasia za pande nyingi na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa ni njia nzuri zaidi ya kuweza kuilazimisha serikali ya Iran iache mpango wake wa nyuklia.

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!