Polisi Ufaransa watumia ukatili kuwafukuza wahamiaji Waafrika
Polisi nchini Ufaransa wametumia ukatili na nguvu ziada kuwafukuza wanawake wahamiaji Waafrika na watoto wao kutoka eneo moja la Paris. Kwa mujibu wa mkanda wa video wa dakika 30 kuhusu tukio hilo la udhalilishaji, Polisi wa Ufaransa wametumia ukatili usio wa kawaida katika kuwafukuza kwa nguvu wanawake na watoto wenye asili ya Afrika katika mtaa wa La Courneuve mjini Paris. Kwa mujibu wa mkanda huo wa Video Polisi ya Ufaransa iliwavua nguo na kuwadhalilisha watoto na wanawake hao waliokuwa wakilia. Wahamiaji wapatao 60 wamefukuzwa bila ilani kutoka nyumba walimokuwa wakiishi. Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yameanzisha kampeni ya kupinga unyama huo wa Polisi nchini Ufaransa. Huku hayo yakijiri Rais Nicholas Sarkozy wa Ufaransa ametangaza mpango wa kufuta uraia wa wahamiaji wa kigeni ambao wanathubutu kukabiliana na polisi nchini humo
0 comments:
Post a Comment