China imefanikiwa kurusha satelaiti ya tano ya kuongoza safari kwenye anga ya juu, ambayo ni ya tatu kurushwa na China kwa mwaka huu. Kwa mujibu wa mpango, Chna itarusha satelaiti zaidi ya 30 za aina hiyo ili kujenga mfumo wa kuongoza safari uitwao Beidou kwenye anga ya juu. Mfumo huo unatarajiwa kuanza kutuika mwaka 2020.
Habari zinasema, mfumo huo ulisanifiwa na China yenyewe. Katika miaka 19 iliyopita, mfumo huo ulitumika katika shughuli za upimaji ramani, mambo ya mawasiliano na uchukuzi, mawasiliano ya simu, uhifadhi wa maji, kazi ya kuzuia na uokoaji wakati wa maafa.
0 comments:
Post a Comment