Waasi wa jimbo la Darfur Sudan na Umoja wa Mataifa leo wametia sahii mkataba wa kuwalinda watoto.
Hatua hii ina lengo la kusitisha utumiaji wa watoto jeshini. Kituo cha mazungumzo ya kijamii kimesema kundi la Justice and Equality Movement JEM na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wametia sahihi makubaliano hayo mjini Geneva. Kama sehemu ya makubaliano hayo kundi la JEM limehakikisha litawaachilia wavulana wote na wasichana walioko kwenye kundi hilo kama wapo na kuwakabidhi kwa UNICEF na pia kusaidia kuwarejesha katika maisha ya kawaida.
Pia limekubali kuwaachia na kuwakabidhi watoto ambao hawajihusishia na JEM moja kwa moja bali kama wapo ambao huenda walikuwa wanatumiwa na makundi mengine katika vita. Zaidi ya hayo JEM limesema litahakikisha linawalinda watoto na masuala ya ukatili wa kimapenzi kama ubakaji.
0 comments:
Post a Comment