Tathimini ya mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia Mark Bowden inasema Somalia ni moja ya matatizo ya kibinadamu yenye utata mkubwa.
Amesema watu takribani milioni 3.2 ambao ni zaidi ya asilimia 40 ya Wasomali wote wanahitaji msaada wa kibinadamu. Mmoja kati ya watoto watano nchini humo wana utapia mlo na Somaliani moja ya nchi the kiwango kikubwa cha utapia mlo duniani. Bwana Bowden anasema kwa sababu ya vita wakimbizi wa ndani milioni 1.2 wanaishi katika mazingira magumu sana.
Ameongeza kuwa raia wanabeba mzigo mkubwa wa vita hivyo ambapo wanashuhudia makombora yakivurumishwa kutoka kila upande kila siku.
0 comments:
Post a Comment