Mawakala wa serikali ya Marekani mashariki mwa jimbo la Virginia, Jumatano walimkamata kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, Zachary Chesser, na kumfungulia mashtaka kwa kusaidia kupeleka vifaa kwa al-Shabab, kundi lenye msimamo mkali wa ki-Islam, ambalo linajaribu kuiangusha serikali dhaifu ya Somalia inayoungwa mkono kimataifa.
Maafisa wa Marekani walisema Chesser, ambaye pia anajulikana kama Abu Talhah Al-Amrikee, alikamatwa Julai 10 wakati akijaribu kupanda ndege kutoka New York kuelekea Uganda, baada ya jina lake kugunduliwa kwenye orodha ya serikali, ya watu waliopigwa marufuku kusafiri.
Habari na Sauti ya Amerika
0 comments:
Post a Comment