Mkutano wa mawaziri wa masuala ya kigeni katika Muungano wa Afrika unaendelea mjini Kampala Uganda.
Agenda kuu ya mkutano huu ni kujadili usalama na amani katika bara hili na pia suala la maendeleo ya kiuchumi
Katika mashauriano ya usalama, mawaziri hao wanatarajiwa kujikita katika nchi ya Somalia na jimbo la Darfur nchini Sudan.
Mawaziri hao wanaokutana katika kikao chao cha kawaida cha 17 cha Baraza la Utendaji la AU.
Mkutano wa Kawaida wa Kumi na Tano wa viongozi wa nchi na wakuu wa serikali wa Afrika unatarajiwa kuanza mjini Kampala, Uganda, Jumapili wiki hii.
Kwa mjibu wa Katibu wa tume ya Muungano wa Afrika Balozi Jean Nfason viongozi ishirini wamethibitisha kuhudhuria mkutano huu na kusema wengine zaidi wanatarajiwa kuthibitisha kabla ya kuanza kwa kikao chao Jumapili wiki hii.
Balozi Nfason amesema tume hiyo imeandaa mpango wa utekelezaji kuhusu namna ya kukabiliana na masuala ya afya ya mama na mtoto ambao utapitishwa na viongozi hao katika mkutano wao.
Mpango huo unalenga kuhakikisha kwamba hakuna mwanamke au mtoto anayekufa kwa kukosa huduma bora ya afya.
Habari na Bbcswahili
0 comments:
Post a Comment