Searching...
Tuesday, July 20, 2010

Raia wa kigeni wajeruhiwa Afrika Kusini

Polisi Afrika Kusini

Polisi Afrika Kusini

Takriban raia wa kigeni wanne wamejeruhiwa katika kitongoji cha Kya Sands nchini Afrika Kusini, mjini Johannesburg katika mashambulio yanayowalenga raia wa nje ya nchi hiyo.

Msemaji wa polisi amesema walikuwa pia wakichunguza taarifa za uporaji.

Mwandishi mmoja wa habari wa Johannesburg alisema maafisa wa polisi walitumia risasi za mpira, gari la kujihami na helikopta ili kuzuia mapigano hayo.

Tangu Kombe la Dunia kumalizika, kumekuwa na wasiwasi wa kuibuka upya mashambulio dhidi ya raia wa kigeni yaliyotokea mwaka 2008.

Takriban watu 62 waliuawa katika vurugu hizo wakati raia wa Afrika Kusini walipowalaumu wafanyakazi wa kigeni kwa kuchukua kazi na makazi yao.

Idara inayotoa huduma za dharura mjini Johannesburg imesema iliwapeleka 'takriban watu watano' hospitalini baada ya kupigiwa simu juu ya ghasia hizo.

Msemaji wa polisi amesema watu wanne walishambuliwa.

Serikali imekuwa ikijaribu kuzima wasiwasi wa kutokea mashambulio dhidi ya raia wa kigeni tangu Kombe la Dunia kumalizika mapema mwezi huu- iliyoandaliwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Maelfu ya wafanyakazi wa muda waliokuwa wamepata ajira wakati wa mashindano hayo wameachishwa kazi tangu imalizike Julai 11.

Mwishoni mwa juma, chama tawala cha African National Congress (ANC) kiliandaa maandamano kupinga mashambulio hayo mjini Johannesburg.

Lakini jitihada zao hazijawazuia watu kuhama na siku ya Jumatatu, serikali ya Zimbabwe imesema itaandaa hifadhi za muda katika maeneo mbalimbali mpakani kwa Wazimbabwe wanaoondoka Afrika Kusini kufuatia vitisho vya kushambuliwa kwa raia wa kigeni.

Madzudzo Pawadyira, mkuu wa idara ya usalama wa raia ameiambia shirika la habari la AFP , " Tumeweka mahema makubwa matatu huko Beitbridge, blanketi 10,000, makasha 20 ya sabuni na ndoo 1,000."

Takriban Wazimbabwe milioni tatu wanaishi Afrika Kusini, baada ya kukimbia kufuatia kudhoofu kwa hali ya uchumi na ghasia za kisiasa nyumbani.

Habari na Bbcswahili

0 comments:

WELCOME URARY95 SPORTS NEWS BLOG | ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A CHEAP PRICE MORE INFORMATION CONTACT US: 0654315901 | Email: urary95@yahoo.com | KARIBU URARY95 SPORTS NEWS BLOG | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI: 0654315901 | Barua Pepe: urary95@yahoo.com
 
Back to top!